Uchaguzi wa Kibra: IEBC yatoa onyo kali dhidi ya usambazaji wa picha za kura

Tume ya IEBC imewaonya wapiga kuzingatia siri za upigaji kura na kukoma kusambaza mtandaoni picha za kura zilizopigwa.

Kupitia mtandao wa Twitter, tume huru ya uchaguzi na na mipaka imeonya kwamba ukiukaji wa sheria hiyo

https://twitter.com/IEBCKenya/status/1192337199087472640?s=20

Hii ni baada ya mpiga kura wa Kibra kupiga picha ya karatasi za kura na kuchapisha katika mtandao wake Alhamisi.

Mpiga kura katika eneo la Kibra baada ya kupiga kura.

Wapigakura walijitokeza asubuhi na mapema katika wadi tano za Kibra huku milolongo mirefu ikishuhudiwa.

Sheria za uchaguzi zinaeleza kuwa kila mtu aliye katika kituo cha kupigia kura anafa kudumisha na kuzingatia sheria ya usiri wa upigaji kura.

Yeyote anayekiuka sheria za siri za kura ni kosa la jina na anaweza kushatkiwa na kuhukumiwa kifungo kisichozidi miaka mitatu au faini ya shilingi milioni moja au yote mawili.

Kiti cha ubunge cha Kibra kiliachwa wazi baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge Ken Okoth.