Kalonzo amelazimishwa kujiunga na Azimio-Jimi Wanjigi adai

Muhtasari
  • Mwanasiasa Jimi Wanjigi amesema kuwa kinara wa ODM Raila Odinga ndiye aliyemshauri kujiunga na siasa
Jimi Wanjigi akizungumza baada ya kujiunga na chama cha Safina 9/Machi/2022
Image: Ezekiel Aming'a

Mwanasiasa Jimi Wanjigi amesema kuwa kinara wa ODM Raila Odinga ndiye aliyemshauri kujiunga na siasa.

Akizungumza Jumatatu, Wanjigi alisema kuwa wakati huo, Waziri Mkuu huyo wa zamani alimweleza kuwa anastaafu kutoka kwa siasa.

“Raila alinishauri nijiunge na siasa, akasema anastaafu, akaniambia kuwa ameisaidia nchi vya kutosha na ni wakati wa kizazi kingine kuchukua hatamu, sijui ni nani, lakini nadhani kuna mtu anamsukuma. " aliiambia NTV.

Mfanyibiashara ambaye hivi majuzi aliidhinishwa kuwania urais kwa tiketi ya chama cha Safina alisema alitofautiana na Raila baada ya chama kumtenga.

Aliongeza kuwa tofauti zake na Waziri Mkuu wa zamani na Rais sio za kibinafsi.

Wakati wa mahojiano, Wanjigi alimshutumu kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka kwa kulazimishwa kufanya kazi na Raila chini ya muungano wake wa Azimio la Umoja.

"Niliwekwa kando na ODM nikaenda kwa rafiki yangu Kalonzo ambaye tulikuwa naye 2017. Tulipokuwa Kitui aliniomba nisimpeleke tena Azimio au Raila Odinga. Ninavyoona analazimishwa kufanya kazi na Azimio, namfahamu."

Wanjigi pia alimshutumu Rais Uhuru Kenyatta kwa kutumia watu wengine kurefusha muda wake mamlakani zaidi ya 2022.

"Tumeandaliwa kwa miaka 60 iliyopita na ni wakati wa wananchi kujipanga. Raila na Ruto wamekuwa kwenye siasa kwa miaka 30 na tumeona walichofanya. Watu wanateseka."