Raila asema hajui chochote kuhusu Ruto kupindua serikali

Muhtasari

• Kinara wa ODM Raila Odinga amesema kwamba hana ufahamu wowote kuhusu njama ya kumuondoa mamlakani rais Uhuru Kenyatta.

• Kauli hii inajiri siku chache baada ya rais Kenyatta kusema kwamba naibu rais William Ruto alikuwa na mpango wa kupindua serikali yake.

Kinara wa ODM Raila Odinga amesema kwamba hana ufahamu wowote kuhusu njama ya kumuondoa mamlakani rais Uhuru Kenyatta.

Kauli hii inajiri siku chache baada ya rais Kenyatta kusema kwamba naibu rais William Ruto alikuwa na mpango wa kupindua serikali yake.

Akizungumza katika mkutano na viongozi wa vyuo vikuu, Odinga alisema kwamba hana lolote la kuzungumzia kuhusu suala hilo.

Jumamosi, rais Kenyatta alifunguka kwa mara ya kwanza kwamba naibu wake alikuwa na mipango ya kumuondoa mamlakani ili achukue nafasi hiyo.

Kenyatta alisema kwamba Ruto alikuwa na tamaa ya uongozi , jambo lililomfanya ampige vita.

Kulingana na rais, hiyo ndo ilikuwa sababu ya kuungana na Raila Odinga mwaka wa 2018 ili kushirikiana katika kuleta maendeleo chini.