Ruto amvulia Uhuru shati amuonya kuacha kuligawanya taifa

Muhtasari

• DP alikuwa akizungumza katika siku yake ya tatu ya kampeni za ukanda wa Pwani ambapo aliongoza washirika wake wa Kenya Kwanza hadi Msambweni, Kwale.

• Bw Rais unajua si kweli ni uongo na ninataka kukuuliza kwa unyenyekevu kulinda ofisi ya rais," Ruto alisema.

• Naibu rais ambaye alionekana kukerwa na kwamba alikuwa amepanga njama ya kumpindua Uhuru.

Naibu rais William Ruto
Naibu rais William Ruto

Naibu Rais William Ruto amemkashifu Rais Uhuru Kenyatta kwa kile alichokitaja kuwa hutumia Ikulu kupanda mbegu za mifarakano na migawanyiko miongoni mwa Wakenya.

Naibu rais ambaye alionekana kukerwa na kwamba alikuwa amepanga njama ya kumpindua Uhuru, Naibu Ruto alimzungumzia Rais Kenyatta moja kwa moja akimtaka rais kuwa ishara ya umoja wa kitaifa badala ya kujihusisha na propaganda.

DP alikuwa akizungumza katika siku yake ya tatu ya kampeni za ukanda wa Pwani ambapo aliongoza washirika wake wa Kenya Kwanza hadi Msambweni, Kwale.

"Tafadhali Bw. Rais, wewe ni kiongozi wa Wakenya wote, usiruhusu Ikulu itumike kama jumba la upanzi wa mbegu za mgawanyiko wa Wakenya," Ruto alisema huku akitaja madai hayo kuwa yasiyo na msingi.

"Bw Rais unajua si kweli ni uongo na ninataka kukuuliza kwa unyenyekevu kulinda ofisi ya rais," alisema.

Ruto yuko katika kinyang’anyiro kikali cha urais na kiongozi wa ODM Raila Odinga ambaye anaungwa mkono na Rais Kenyatta.

“Hata kama hutaki kuniunga mkono... ni sawa, nilikuunga mkono bila masharti, rafiki yangu mheshimiwa Rais naomba usiruhusu Ikulu iwe uwanja wa kuenezwa uongo, propaganda na ukabila hasi dhidi yangu. kama naibu wako. Rafiki yangu nilisimama nawe wakati hakuna mtu mwingine aliyekuwa tayari kusimama nawe...," Ruto alisema.

Siku ya Jumamosi, Rais Uhuru Kenyatta anadaiwa kuzungumza kwa mara ya kwanza kuhusu njama ya naibu wake, William Ruto, kutaka kumwondoa madarakani kupitia kura ya kutokuwa na imani na kuhujumu mipango ya serikali.

Kenyatta, ambaye alikuwa akiwahutubia wazee wa Gìkùyù waliomtembelea Ikulu, Nairobi alisema Ruto alikuwa na uchu wa madaraka na alikuwa na nia ya kuibua upinzani kutoka ndani ya chama cha Jubilee, ili kumuondoa madarakani.

Rais pia alichukua muda kuwaeleza wazee kwa nini aliamua kumpigia debe kinara ya upinzani ODM Raila Odinga na kukubali Handshake mwaka 2018.