Robert Alai ataja sababu ya kusalimu amri ubunge wa Nyando kuwania MCA Kileleshwa

Muhtasari
  • Robert Alai ataja sababu ya kusalimu amri ubunge wa Nyando kuwania MCA Kileleshwa
Robert Alai
Image: Facebook

Mwanablogu Robert Alai ametangaza rasmi kwamba atawania kiti cha MCA katika wadi ya Kileleshwa katika uchaguzi wa Agosti 9.

Alai atawania wadhfa huo kupitia tikiti ya chama cha ODM.

Kupitia ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Facebook, Alai alisema kwamba uamuzi huo ulijiri baada ya mashauriano na chama cha ODM.

Akizungumza na Mpasho, Robert alieleza kuwa kwa wakati huu, ataleta athari zaidi kama mbunge anayewakilisha wakazi wa jiji.

Anasema kuwa kubadilisha Nairobi kutaleta mabadiliko katika maeneo makubwa ya nchi.

"Ukisema umeonyesha nia ya kugombea ubunge hivyo huwezi kwenda kwa MCA hausaidii Wananchi. Ni faida ya ubinafsi na inaonyesha ulitaka kukidhi nafsi yako

"Nimekaa katika jiji hili kwa muda mrefu na ukimuuliza mtu wa Nyayo Estate Embakasi ambapo nilikuwa Mwenyekiti kwa muda utaelewa kuwa nilileta mabadiliko mengi huko," alisema.

Wakati wa utumishi wake kama Mwenyekiti wa Estate, Robert anasema alileta utaratibu mwingi kwenye makao ambayo hupokea wakaaji karibu 5,000.

"Niligundua kuwa watu sio lazima wapiganie haki zao moja kwa moja...kuna watu unaowachagua kukuwakilisha na kueleza masuala yako."

Aliwasihi yeyote anayetilia shaka uaminifu wake kwenda Nyayo Estate na kuuliza yeyote pale kwa nini wanampeza.

Robert alielezea mojawapo ya ahadi zake za kuifanya kata ya Kileleshwa kuwa salama na yenye starehe kwa wakazi wote, hasa kuwa na huduma za kijamii.

"Ukiangalia Kileleshwa, kuna maghorofa mengi yanakuja, viwanja vya kuchezea viko wapi? Njia ya kutembea iko wapi? Unahakikishaje wakazi hawa wanaishi kwa raha?"