Mwenyekiti wa UDA, Muthama ajipata vitani na Atheists kwa matamshi yake dhidi ya Raila

Muhtasari

• Tumeyapata matako yako (Muthama) kuwa mabaya na yasiyoweza kuvumilika kwa watu wasiomuamini Mungu. Tunataka msamaha wa hadharani mara moja,” Barua ya Atheists ilisoma.

Mwenyekiti wa UDA, Johson Muthama
Mwenyekiti wa UDA, Johson Muthama
Image: Twitter

Kundi la watu wasioamini uwepo wa Mungu nchini Kenya, Atheists Society, wameandikia mwenyekiti wa chama cha UDA Johnson Muthama barua ya kumtaka kuomba msamaha mara moja kutokana na matamshi aliyoyasema juzi katika mkutano wa kampeni za kisiasa za chama hicho huko Kitui.

Katika kile ambacho rais wa kundi hilo Harrison Mumia alisema kwamba ni matamshi ya kubagua watu wasio na dini, Kundi hilo lilisema kwamba Muthama alikiuka haki za watu wasiotambua dini yoyote kwa kusema kwamba mtu bila dini hawezi pata kiti cha kisiasa.

“Na kamwe hupati uongozi wa Kenya ukiwa mkosa dini,” Muthama alisikika akisema hivo, katika kauli ambayo inadaiwa alikuwa anamlenga kinara wa ODM Raila Odinga.

Mumia aliandikia chama cha UDA waraka wa kutaka mwenyekiti wake huyo kuomba radhi mara moja tena hadharani kwani katiba inaruhusu mtu yeyote kuwania siasa popote bila kujali dini.

“Kundi letu limesajiliwa kikatiba na tunafanya kazi kutetea haki za watu wasiomuamini Mungu nchini Kenya. Tumeyapata matako yako (Muthama) kuwa mabaya na yasiyoweza kuvumilika kwa watu wasiomuamini Mungu. Tunataka msamaha wa hadharani mara moja,” Barua hiyo ilisoma.

Hapa boti la Muthama limeenda mvange baada ya tombwe lake lililolenga kumfuma Raila kupoteza dira na kutua kwenye ardhi ya wasioamini Mungu.

Image: TWITTER