Gavana Lee Kinyanjui kutetea kiti chake cha ugavana kwa tikiti ya Jubilee

Muhtasari
  • Gavana Lee Kinyanjui kutetea kiti chake cha ugavana kwa tikiti ya Jubilee
Gavana wa Nakuru Lee KInyanju
Image: MAKTABA

Gavana wa kaunti ya Nakuru Lee Kinyanjui kupitia kwenye ukurasa wake wa Twitter, ametangaza kwamba atatetea kiti chake cha ugavana  kwa tikiti ya JUbilee katika uchaguzi mkuu ujao.

Gavana alitoa tangazo hilo siku ya Ijumaa na kusema kuwa hatua hiyo ni kuunganisha kituo cha usaidizi cha Azimio La Umoja kabla ya uchaguzi wa Agosti 9.

“Ili kuunganisha msingi wa usaidizi wa Azimio Coalition na kuongoza timu ya kampeni katika eneo hili, uamuzi umefika kwamba nitetee kiti changu cha Ugavana kwa tikiti ya Jubilee Party. Kwa hivyo, ningependa kueleza kwamba nitatetea kiti changu cha Ugavana wa Nakuru kwa tikiti ya Jubilee,” Kinyanjui alisema.

Kinyanjui alisema uamuzi huo umetolewa baada ya mashauriano na uongozi wa juu na wanachama wa chama cha Ubuntu peoples forum.

Hapo awali alisema atawania kuchaguliwa tena kwa tiketi ya chama cha Ubuntu.

"Wakati huo huo, chama cha UPF kitasimamisha na kumuunga mkono mgombeaji wake katika nyadhifa husika kulingana na mamlaka yake," Kinyanjui alisema.

Kinyanjui alisema sasa watakaribia uchaguzi wa Agosti 9, kama timu ya Azimio la Umoja.