OKA yaungana na Azimio kuunda Azimio la Umoja - One Kenya Alliance

Muhtasari

• Maamuzi haya yaliafikiwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu.

• Walikubaliana kumuunga mkono Raila Odinga kama mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Star, KWA HISANI
Star, KWA HISANI
Image: Viongozi wa muungano wa Azimio la Umoja - One Kenya Alliance

Hatimaye mrengo wa OKA umesaini mkataba na kuingia  katika makubaliano na vuguvugu la Azimio kuunda muungano wa Azimio la Umoja - One Kenya Alliance.

Sasa muugano huo mpya utasajiliwa kuwa chama rasmi cha kisiasa.

Wakizungumza na wanahabari, makatibu wakuu wa vyama tanzu chini ya muugano huo walikubaliana kushirikiana katika azma ya kuhakikisha Raila Odinga anaibuka kidedea katika uchaguzi wa urais, Agosti 9.

Walisema kwamba uamuzi huo uliafikiwa baada ya mazungumzo ya kina miongoni mwa vyama hivo.

Hatua hii inamaaisha kwamba vyama tanzu vitakuwa na usemi katika muungano huo na kwamba matakwa yao lazima yataagaziwa a kushughulikiwa.

Kuhusu swala la mgombea mwenza, walisema kwamba atachaguliwa kutoka kwa chama chochote kilichopo chini ya mwavuli huo.

Kulingana nao sasa kutaandaliwa misururo ya kampeni katika maeneo yote nchini ili kuuza sera zao huku wakianza na kaunti ya Pokot Magharibi siku ya Jumamosi.

Aidha, sasa kutakuwa na mikutano ya mara kwa mara kuhakikisha kwamba wanajadili mbinu za kufanikisha mipango yao mbele ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Vilevile waligusia kwamba watazidi kupambana kuhakikisha mswada wa BBI uapitishwa na kuwa sheria.

ikumbukwe kwamba kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka alikuwa ameshikilia kwamba lazima angekuwa debeni katika kivumbi hicho ila sasa ni rasmi kwamba atakuwa anamuunga mkono Raila Odinga.