Ruto tu ndo unaweza kuamini, Kuria amwambia Kalonzo

Muhtasari

• Moses Kuria amemtaka Kalonzo kushikana mkono na aibu rais William Ruto baada ya BBI kuangushwa.

• Amesema kwamba Ruto ndo tu ambaye anaweza kuaminika na Kalonzo.

Mbunge wa Gatundu kusini Moses Kuria amemtaka kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka kumuamini naibu rais William Ruto wakati huu ambapo mswada wa BBI umetupiliwa mbali.

Kupitia taarifa yake siku ya Ijumaa, Kuria alisema kwamba Kalonzo hawezi kuwa na imani kwa kinara wa ODM Raila Odiga ikifahamika kwamba mahakama ya upeo iliangusha BBI.

Kuria alimtaka Kalonzo kumuamini Ruto kwani yeye ni muungwana ambaye anadumisha ahadi yake.

"Rafiki yangu Kalonzo Musyoka habari ya asubuhi. Mugu bado anakupenda. Sasa ambapo huwezi kumuamii Raila Odinga bila BBI, ni wakati mzuri umuamini mtu ambaye anatekeleza mambo kulingana na ahadi zake kama William Ruto," Kuria alisema.

Kauli hii inajiri siku moja baada ya Kuria kusema kwamba angeunga mkoo BBI iwapo mahakama ya upeo ingeamuru mchakato huo kuedelea mbele.

Alisema kwamba tatizo la mswada huo lilikuwa kwamba haukufuata hatua za kisheria.

Mahakama ya upeo siku ya Alhamisi ilipiga msumari wa mwisho kwenye jeneza la BBI, mswada ambao ulikuwa unalenga kufanya marekebisho katika vipengele  kadhaa vya katiba.