Kalonzo kuwa mgombea mwenza wa Raila katika uchaguzi ujao

Muhtasari
  • Kalonzo kuwa mgombea mwenza wa Raila katika uchaguzi ujao
Seneta wa kaunti ya Makueni Mutula Kilonzo
Image: Enos Teche

Seneta wa Makueni Mutula Kilonzo Junior amewaambia wanachama wa Wiper Party kwamba Kalonzo Musyoka atakuwa mgombea mwenza wa Raila Odinga katika kura zijazo.

Mutula aliambia mkutano wa wawaniaji wa chama hicho kwamba tayari kuwa Kalonzo atakuwa naibu mkuu wa ODM na kwamba ilikuwa ni suala la muda kabla ya kufichuliwa.

“Nataka kuwaambia kuwa naibu rais ajaye atatoka Wiper,” alisema.

Makamu mwenyekiti wa Wiper pia aliwataka wagombeaji kutohama chama baada ya uteuzi iwapo watashindwa.

"Kwa sababu baada ya yote, hiki ni chama cha serikali,Muunge mkono anayeshinda kwa sababu ukiwa serikalini, wote mtakubaliwa," alisema.

Alisema chama hicho kilitaka kuimarisha mkono wa Kalonzo katika mechi yake ya kuwania madaraka na Raila kwa kushinda viti zaidi.

"Hakuna haja ya kuwa na Kalonzo kuwa naibu wa rais lakini kuwa na viti vichache. Tunataka kupata fedha za chama cha siasa."