"Ni Bottoms-Up!" Moses Kuria ainua 'boxer' na kupigwa picha nayo sokoni, kina mama waachia furaha tele

Muhtasari

• Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria aliwaacha kina mama vinywa wazi na vicheko  baada ya kuinua 'boxer' ya wanaume juu akipiga kampeni sokoni.

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria
Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria
Image: Facebook

Mbunge wa Gatundu ya Kusini Moses Kuria amegeuka gumzo la mitandaoni baada ya kuonekana akipeperusha mwanandani ya kiume almaarufu ‘boxer’ hewani wakati akiwa katika ziara ya kukitangaza chama chake cha Kazi na kujipigia debe kama gavana ajaye wa Kiambu.

Katika msururu wa picha ambazo mbunge huyo alizipakia kwenye ukurasa wake rasmi wa Facebook pamoja na ukurasa wa Chama Cha Kazi, Kuria anaonekana akitaguzana na bidhaa mbalimbali sdokoni huku akichukua picha na wakaazi wenye furaha ya kukutana naye.

Lakini picha moja inayomuonesha akiwa ameinua ‘boxer’ juu tena kwa mikono yote miwili imewaacha wengi katika kicheko kikubwa huku ikiwa bado haijajulikana kama alikuwa anapiga biashara ya kutaka kuinunua ama alikuwa anaionesha kwa umati kwa nia gani.

Mbunge huyo anayeegemea mrengo wa naibu rais William Ruto, Jumatano alipeleka kampeni zake katika maneneo mbalimbali ya kaunti ya Kiambu yakiwemo maeneo ya Gikambura, Lusigiti, Mutarakwa, Limuru miongoni mwa sehemu nyingine kwenye kaunti pana ya Kiambu.