Bahati aongoza kwa 35.2% huko Mathare - Kura ya maoni

Muhtasari

• Msanii Bahati anaonekana kuongoza kwa umaarufu katika eneobunge la Mathare.

• Ndo mara yake ya kwanza kuingia katika siasa.

Bahati
Bahati
Image: Instagram, KWA HISANI

Msanii Kevin Kioko almaarufu Bahati anaongoza kwa asilimia 35.2 kwa umaarufu katika eneobunge la Mathare.

Anafuatwa kwa ukaribu na mbunge wa sasa  Anthony Oluoch ambaye ana asilimia 32.7.

Wanjohi GM anafunga orodha ya tatu bora huku akiwahi asilimia 18.5 ya kura.

Bahati alionyesha furaha yake kwa kile alichokitaja kama wakazi kuaminia ndoto yake ya kubadilisha maisha yao na kuwaletea maendeleo.

" Mathare imeamua.Kura ya maoni inaonyesha kwamba iwapo uchaguzi ungefanyika hii leo Bahati angekuwa mbunge wa eneo la Mathare," Bahati aliandika.

Ifahamike kwamba ndo mara ya kwanza kwa msanii huyo kuwania wadhifa wa uongozi nchini.

Anajiunga na orodha ya wasanii na mastaa mbalimbali ambao wameamua kujitosa katika kivumbi cha Agosti 9.