Fahamu mwanasiasa anayepiga kampeni za ugavana kwa kutumia baiskeli

Muhtasari

• Solomon Kiptarbei Maritim, mkaazi wa kaunti ya Uasin Gishu huko bonde la ufa amekiuka miiko mingi ya kisiasa ambapo ameamua kupiga kampeni zake za ugavana kwa kutumia baiskeli.

Solomon Kiptarbei Maritim, jamaa anayepiga kamppeni za ugavana kwa baiskeli
Solomon Kiptarbei Maritim, jamaa anayepiga kamppeni za ugavana kwa baiskeli
Image: Facebook, Uasin Gishu News

Solomon Kiptarbei Maritim, ni mwanaume mmoja mwenye ameamini kwamba siasa ni sera wala si pesa na magari ya kifahari.

Mwanaume huyu mkaazi wa kaunti ya Uasin Gishu huko bonde la ufa amekiuka miiko mingi ya kisiasa ambapo ameamua kupiga kampeni zake kwa kutumia baiskeli.

Wengi wanamtambua kama Gavana wa Baiskeli kutokana na matumizi yake ya chombo hicho cha usafiri akizunguka katika maeneo kadhaa ya kaunti hiyo pana huku akijipigia debe kuwa mrithi wa gavana Jackson Mandago katika uchaguzi ujao wa Agosti 9.

Maritim ambaye ana shahada ya masuala ya fedha kituko chuo kikuu cha Moi alijaribu bahati yake ya kwanza kuwa gavana wa Uasin Gishu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2017 ambapo kura za maoni kipindi kile zilikuwa zinamuweka nambari 3, nyuma ya gavana Jackson mandago na mfanyabiashara maarufu Zedekiah Bundotich almaarufu Buzeki.

Kwa jamaa huyu mwenye ujuzi wa kufanya mipangilio ya matumizi ya fedha, kuwa na timu katika kampeni ni kutu cha kipuuzi ambamo yeye anaamini kwa kupiga debe na kuzitangaza sera zake peke yake, jeshi la mtu mmoja hili!

Wakati mmoja aliwahi ulizwa sababu zake za kutumia baiskeli katika kampeni zake hali ya kuwa washindani wake wakuu wanatumia misafara mirefu tena ya magari ya kifahari na iwapo jambo hilo halimpi kiwewe, Maritim alisema kwamba katika uchaguzi uliopiga baada ya washindane wake kujua kwamba sera zake zinawiana na mambo ya mwananchi wa kawaida, walianza kumpiga vita kwa kusema kwamba anafanya tu mzaha na wala hana lengo la kuwania kiti hicho.

Mwanasiasa huyo mwenye njia ya kipekee ya kupiga kampeni alisema kwamba baiskeli yake ameitumia enzi akiwa shule ya upili ambapo ilimsaidia kwa miaka minne katika safari za shuleni na kuwataka wakaazi wa Uasin Gishu kumpigia kura kwani yeye hatumii chombo hicho ili kutafuta kura za huruma.

Maritim mwenye umri wa miaka 35 alisema licha ya kuwa na shahada, kamwe hajawahi ajiriwa, sawia tu na mamia ya watu wenye shahada.