(RIP) Mwanasiasa Wesley Kogo afariki kwa ajali ya barabarani miezi 3 tu baada ya harusi yake

Muhtasari

• Mwanasiasa huyo alipata ajali katika eneo la Kangemi kuingia Nairobi ambapo alikuwa anatarajiwa kufanya mahojiano ya kipekee na kituo kimoja cha redio jijini Nairobi.

• Kifo cha mwanasiasa huyo mchanga kinatokea takribani miezi mitatu tu baada ya kufunga harusi ya kufanya na mpenzi wake.

Mwaniaji wa kiti cha ubunge Nandi Hills, Weslay Kogo
Mwaniaji wa kiti cha ubunge Nandi Hills, Weslay Kogo
Image: Facebook

Weslay Kogo, mwanasiasa aliyekuwa analenga kiti cha Ubunge wa Nandi Hills kwa tiketi ya chama cha UDA ameaga dunia kupitia ajali mbaya ya barabarani.

Taarifa zinasema kwamba mwanasiasa huyo alipata ajali katika eneo la Kangemi kuingia Nairobi ambapo alikuwa anatarajiwa kufanya mahojiano ya kipekee na kituo kimoja cha redio jijini Nairobi.

Kifo cha mwanasiasa huyo mchanga kinatokea takribani miezi mitatu tu baada ya kufunga harusi ya kufanya na mpenzi wake.

Kogo alikuwa na azma ya kushinda kiti cha ubunge wa Nandi Hills kwa kumuangusha mbunge wa sasa Alfred Keter.

Mwanasiasa huyo mchanga awali alikuwa amewaomba watu kumchangia ili kupata hela za kufadhili kampeni zake ambapo kwa mshtuko wa wengi, mchango huo ulifanikiwa pakubwa ambapo alifanikiwa kuchangisha zaidi ya milioni 1.6 pesa za Kenya, lakini kwa bahati mbaya ndoto yake ya kuongoza wananchi wa Nandi Hills zilitumbukia gizani kwa ajali ya barabarani ambapo alikuwa akitumia usafiri wa magari ya umma.