"Kila la Kheri UDA katika mchujo wenu" - Babu Owino

Muhtasari

• Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino amewatakia kila la kheri wapinzani wake wa UDA katika uchaguzi wa mchujo Alhamis.

Babu Owino, mbunge wa Embakasi East
Babu Owino, mbunge wa Embakasi East
Image: Babu Owino////Facebook
Babu Owino, mbunge wa Embakasi East
Babu Owino, mbunge wa Embakasi East
Image: Babu Owino////Facebook

Mbunge wa Embakasi ya Mashariki, Babu Owino kwa mara ya kwanza ameonesha siasa komavu baada ya kuamua kuweka tofauti za kisiasa kando na kuwatakia kila la kheri washindani wake kutoka chama cha UDA, wanaoenda debeni Alhamis kwa mchujo wa kuwania tiketi ya chama hicho ili kupambana naye katika ubunge Embakasi Mashariki.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Babu Owino aliandika kwamba hana chuki nao kwa sababu anajua hakuna hata mmoja kati ya wale wanaogombea tiketi ya UDA atambwaga katika kikitetea kiti hicho cha Embakasi Mashariki mnamo Agosti 9.

Babu Owino analenga kuitetea nafasi hiyo kupitia chama cha ODM ambacho ni mwanachama mkuu na mwasisi wa mrengo wa Azimio la Umoja unaonngozwa na Raila Odinga ambaye watamenyana katika kiti cha urais na kiongozi wa UDA William Ruto miongoni mwa wagombea wengine.

“Ningependa kuchukua nafasi hii kuwatakia wapinzani wangu WASIOSTAHILI UDA katika Jamhuri ya Embakasi Mashariki kila la kheri katika uchaguzi wao wa Mchujo wa Chama kesho. Nitawashinda mapema saa kumi na moja asubuhi tarehe 9/8/2022,” aliandika Babu Owino.

Chama cha UDA kinatarajiwa kufanya kura za mchujo kote nchini Alhamisi tarehe 14 mwezi huu wa Aprili.

Kila la Kheri kwa wote wanaolenga tiketi za chama hicho kuwania nyadhifa mbalimbali.