Mgombea MCA kwa tiketi ya UDA ashambuliwa na wahuni katika kituo cha kupigia kura cha Mathare

Muhtasari
  • Mgombea MCA kwa tiketi ya UDA ashambuliwa na wahuni katika kituo cha kupigia kura cha Mathare
MGOMBEA MCA ELIZABETH WAITHERA
Image: GEORGE OWITI

Mgombea uwakilishi wadi wa UDA amejeruhiwa baada ya kushambuliwa na wahuni wakati wa mchujo wa chama unaoendelea katika eneo bunge la Mathare.

Elizabeth Waithera, 39, alivamiwa na nguo zake kuraruliwa na wahuni anaodai kuwa ni za mpinzani wake katika shule ya msingi ya Kiboro jijini Nairobi mnamo Alhamisi.

Waithera ni miongoni mwa wagombeaji wanaoshiriki uchaguzi wa mchujo wa UDA unaoendelea.

Anagombea kata ya Mlango Kubwa. Ni wawaniaji wanne wa kiti hicho wanaokipigania kwa tikiti ya chama cha UDA.

Waithera aliripoti kisa hicho katika kituo cha polisi cha Pangani kama kesi ya shambulio kwenye OB NO. 75/14/4/22 saa 1010.

Alisema alikuwa amenyimwa ufikiaji wa kituo cha kupigia kura na kwa hivyo hakuweza kupiga kura yake mwenyewe.

"Mimi ni mgombeaji katika wadi ya Mlango Kubwa ninayegombea MCA na kushiriki katika uteuzi unaoendelea wa UDA na nimenyimwa haki ya kupiga kura," Waithera aliambia Radiojambo mnamo Alhamisi.

Waithera alisema hakuweza kufikia vyumba vya madarasa ambapo zoezi la uteuzi lilikuwa likiendelea shuleni hapo.

"Majambazi hao ni wa mmoja wa wapinzani wangu ambaye pia anashiriki uchaguzi wa mchujo. Walininyanyasa, kunirarua nguo na hata kuninyanyasa kingono," Waithera alisema.

"Hawajaniruhusu kupiga kura hata sasa. Sina mtu wa kutafuta suluhu kwa vile hata sina afisa msimamizi katika kituo cha kupigia kura," Alisema.

Waithera alisema maafisa wa polisi wanaosimamia kituo hicho walimpuuza. Walitazama jinsi alivyoshambuliwa na hawakufanya chochote kuhusu hilo.

Alidai kuwa wahalifu hao walichukua kituo cha kupigia kura.

Waithera alitaka haki itendeke. Anataka mamlaka husika kuingilia kati ili atumie haki yake ya kupiga kura.

Pia anataka polisi kuchukua hatua kwa washambuliaji wake na wafadhili wao.

Waithera aliitaka bodi ya kitaifa ya uchaguzi ya UDA kuchukua jukumu la uteuzi na kuhakikisha uteuzi huru na wa haki.

Anataka timu ya usalama kutoka eneo hilo kutoa ulinzi kwa wanaotaka.

Inaisha...