(VIDEO) Karatasi za kupiga kura za mchujo UDA zachomwa Embu

Muhtasari

• Karatasi za kupiga kura za mchujo wa chama cha UDA zilizokuwa zikisafirishwa kwenda Embu zilichomwa na kundi la vijana.

Naibu wa rais William Ruto
Naibu wa rais William Ruto
Image: Maktaba, Screenshot

Chama cha naibu rais William Ruto, UDA kilipata pigo la karne Jumatano jioni baada ya watu huko Embu kuchoma karatasi na stakabadhi za kura za mchujo zilizokuwa zinatarajiwa kufanyika Alhamis.

Katika moja ya video ambazo zilisambazwa pakubwa kwenye mitandao ya kijamii, vyombo hivyo vya kuandaa kura ya mchujo ya chama hicho vilitiwa moto na vijana waliokuwa wakilalamikia madai ya uwezekano wa kuibiwa kwa mura hizo kwa baadhi ya wagombea wanaopendelewa na viongozi wakuu chamani.

Kulingana na madai yaliyoibuliwa na vijana hao ni kwamba karatasi zilizokuwa zikisafirishwa katika vituo mbalimbali zilikuwa tayari zimetiwa alama kama njia moja ya kufanya uchaguzi kwa upendeleo wa baadhi ya wanasiasa.

Baadae mwenyekiti wa kitaifa anayesimamia chaguzi za chama hicho alidhibitisha kisa hicho na kusema kwamba uchaguzi huo wa mchujo ungeendelea Alhamis 14, kama ulivyokuwa umepangwa na kuratibiwa.

Madai hayo ya wizi wa kura za mchujo chamani UDA yanakuja miezi kadhaa tu baada ya naibu rais William Ruto kutoa hakikisho mara kadha katika hafla na mikusanyiko ya kisiasa kwamba chaguzi hizo zitakuwa za uwazi na haki kote nchini.