'Unaelewa mahitaji ya watu,'Anerlisa Muigai ampongeza mama yake kwa ujumbe wa kipekee

Muhtasari
  • Tabitha alitangazwa kuwa mpeperushaji bendera wa UDA katika kiti cha useneta wa Kaunti ya Nakuru
  • Miongoni mwa waliojitokeza kumpongeza ni bintiye, Arnelisa Muigai

Muungano wa United Democratic Alliance, UDA umekuwa ukifanya uteuzi wa vyama kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti.

Tabitha Karanja alitokea kuwa mmoja wa washiriki wa uteuzi wa UDA na kwa bahati nzuri aliibuka mshindi katika uteuzi wa useneta wa kaunti ya Nakuru.

Tabitha alitangazwa kuwa mpeperushaji bendera wa UDA katika kiti cha useneta wa Kaunti ya Nakuru.

Miongoni mwa waliojitokeza kumpongeza ni bintiye, Arnelisa Muigai.

Arnelisa alimwandikia mamake ujumbe wa kumpongeza na pia kuchukua hatua ya juu kutaja kwamba anamwamini.

Kulingana na Arnelisa mamake atakuwa seneta bora zaidi kuwa kaunti ya Nakuru.

Arnelisa alitaja kwamba mamake anaelewa kikamilifu mahitaji ya watu wa Kaunti ya Nakuru, na kumweka katika nafasi nzuri ya kuwatumikia kama kiongozi wao.

Akiwa mjasiriamali aliyefanikiwa, matamshi ya Arnelisa ni chachu kwa mama yake anapoendelea na kampeni zake.

"Hongera mama, sina shauku kwamba  utakuwa seneta bora, unaelewa kikamilifu mahitaji ya watu," Aliandika Anerlisa.