Kalonzo amkabidhi Mike Sonko tikiti ya moja kwa moja kuwania ugavana wa Mombasa

Muhtasari
  • Kalonzo ampa Mike Sonko tikiti ya moja kwa moja kuwania ugavana wa Mombasa
Image: Hisani

Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amekabidhi tikiti ya chama kwa mwaniaji ugavana wa Mombasa Mike Sonko.

Akizungumza katika kikao na wanahabari siku ya Alhamisi, Kalonzo alisema hatua hiyo ni baada ya maafikiano Sonko na Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo.

"Tumeafikiana kati ya wagombea wetu wawili wanaowania kuwa magavana katika Kaunti ya Mombasa," Kalonzo alisema.

Alisema mbunge wa Kisauni alikubali kuachia ngazi kwa Sonko, na sasa atachukua nafasi ya naibu.

Sonko anataka kumrithi Hassan Joho.

Mapema mwezi jana gavana huyo wa zamani wa Nairobi, Mike Sonko alitangaa kwamba amejiunga na chama cha wiper