Abdulswamad Nassir aongoza kura ya maoni kwa ugavana wa Mombasa

Muhtasari

• Utafiti huo ulifanywa Aprili 2022, na kuchukua sampuli za wahojiwa 1949 katika kaunti za Nairobi, Makueni na Mombasa, na ulikuwa na asilimia 4 ya kasoro.

Iwapo uchaguzi ungefanyika leo, Mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir atamrithi Gavana Hassan Joho, huku aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko akimaliza katika nafasi ya pili.

Kulingana na kura ya maoni iliyotolewa na shirika la Tifa Nassir ndiye mgombeaji maarufu wa ugavana kwa asilimia 40 akifuatwa na aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko kwa asilimia 28.

Utafiti huo ulifanywa Aprili 2022, na kuchukua sampuli za wahojiwa 1949 katika kaunti za Nairobi, Makueni na Mombasa, na ulikuwa na asilimia 4 ya kasoro.