Ruto asema Raila ni mfisadi, amtaka kuajibikia kashfa ya KEMSA

Muhtasari

• Naibu Rais William Ruto amemtaka Kiongozi wa ODM Raila Odinga kustaafu na kurudi nyumbani. 

• “Yeye (Raila) hana uwezo wa kupambana na ufisadi. Yeye ni mfisadi,” Ruto alisema.

• Hapo awali, Ruto aliongoza Kongamano la Kiuchumi la Kaunti ya Busia mjini Nambale.

Image: @WilliamsRuto/Twitter

Naibu Rais William Ruto amemtaka Kiongozi wa ODM Raila Odinga kustaafu na kurudi nyumbani. 

Ruto Alisema Odinga hana ujuzi na uwezo wa kuleta mabadiliko yoyote ya maana nchini. Ruto alisema ‘Handshake’ ilifichua kiongozi huyo wa upinzani kama dereva mahiri wa ufisadi nchini Kenya. 

“Sasa, tunajua rangi halisi za Raila; anawasafisha wafisadi haswa katika kaunti,” Ruto alisema. 

Alimtaka Raila kuwajibikia pesa zilizoibwa katika kashfa ya Mamlaka ya Ugavi wa Dawa nchini Kenya (KEPSA). 

“Yeye (Raila) hana uwezo wa kupambana na ufisadi. Yeye ni mfisadi.” 

Kinara wa ANC Musalia Mudavadi (Kulia) akihutubia wananchi wa Busia akiwa na kiongozi wa Ford Kenya Moses Wetangula.
Kinara wa ANC Musalia Mudavadi (Kulia) akihutubia wananchi wa Busia akiwa na kiongozi wa Ford Kenya Moses Wetangula.
Image: @WilliamsRuto/Twitter

Naibu Rais alikuwa akizungumza siku ya Ijumaa katika maeneo ya Mumias Magharibi, Lurambi na Kabuchai ambako alifanya misururu ya mikutano ya hadhara. 

Hapo awali, aliongoza Kongamano la Kiuchumi la Kaunti ya Busia mjini Nambale ambalo lilihudhuriwa na Viongozi wa Chama Musalia Mudavadi (ANC), Moses Kuria (Chama Cha Kazi) na Moses Wetang’ula (Ford Kenya). 

Pia walikuwepo Spika wa Seneti Ken Lusaka, Wabunge Didmus Barasa (Kimilili), Dan Wanyama (Webuye Magharibi), Mwambu Mabonga (Bumula), Catherine Wambilianga (Bungoma), Majimbo Kalasinga (Kabuchai), Fred Kapondi (Mt Elgon), Chris Wamalwa ( Kiminini), Sakwa Bunyasi (Nambale), Benjamin Washiali (Mumias Mashariki) na Cleophas Malala (Kakamega). 

Naibu Rais alisema Kenya Kwanza ina mikakati ya kuimarisha biashara zisizo rasmi mpakani ili kusaidia wananchi kujiendeleza kiuchumi. 

Image: @WilliamsRuto/Twitter

"Tutaweka wafanyabiashara wadogo katikati ya agenda yetu ya maamuzi na kuanzisha sera zinazounga mkono biashara ambazo zitachochea ukuaji wao," aliwaambia watu wa Busia. 

Kinara wa ANC Musalia Mudavadi alimwomba Rais Uhuru Kenyatta kuwajibikia gharama ya juu ya maisha. 

“Kwa miaka miwili, hamjaitisha kikao cha Baraza la Mawaziri. Je, unatarajiaje kufanya maisha yawe rahisi kwa mamilioni ya Wakenya?” Alisema Mudavadi.