DP Ruto ajipigia debe Trans-Nzoia

Muhtasari

•DP Ruto anatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara kwenye eneo la Matunda Kaunti ya Uasin Gishu.

Image: FACEBOOK// WILLIAM RUTO

Mgombea wa wadhifa wa urais kwenye Muungano wa Kenya Kwanza, Daktari William Ruto amewasili katika Kanisa  Katoliki la St. Peter's Clever Kiminini.

Ruto ameandamana na Spika Wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi,Kinara wa ANC Musalia Mudavadi, Kiongozi wa Chama cha FORD Kenya, Moses Wetangula, Gavana wa Kaunti ya Trans Nzoia, Patrick Khaemba,  Mbunge wa Bumula, Mwambu Mabonga, Mbunge wa Kiminini, Daktari Chris Wamalwa, Ferdinad Wanyonyi wa Kwanza na Daktari Robert Pukose wa Endebess miongoni mwa viongozi wengine.

Misa inaongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Kitale, Anthony Mourice Clowrey.

Baaada ya ibada hiyo Ruto na viongozi wa Muungano wa Kenya Kwanza ataongoza kongomano la kiuchumi kuyakusanya maoni ya wakazi kufanikisha maendeleo ikiwa atachaguliwa kuwa Rais wa tano wa taifa hili.

Mwendo wa saa nane na nusu hivi anatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara kwenye eneo la Matunda Kaunti ya Uasin Gishu.