Nina matumaini mwanangu atakuwa naibu wa Ruto- babake Kindiki

Muhtasari
  • Daniel Kindiki, babake seneta wa Tharaka Nithi Kithure Kindiki, amesema ana matumaini kuwa mwanawe atatajwa kuwa mgombea mwenza wa Ruto

Daniel Kindiki, babake seneta wa Tharaka Nithi Kithure Kindiki, amesema ana matumaini kuwa mwanawe atatajwa kuwa mgombea mwenza wa Ruto.

Katika mahojiano kwenye na KTN Jumamosi, alisema kuwa Kindiki amekuwa na hamu ya kutumikia nchi kwa hadhi ya juu na alihisi huu ulikuwa wakati mwafaka kwani ujuzi wake wa uongozi umethibitisha kuwa ana uwezo.

Alipoulizwa alihisi vipi kuhusu kuchaguliwa kuwa mgombea mwenza, alisema anajua kwamba amehitimu na ana kile anachohitaji kuongoza nchi katika ngazi hiyo. “Ninamuamini, na kwa vile ndivyo alivyokuwa akitaka, nina imani atachaguliwa,” alisema.

Aidha alieleza kuwa Kindiki ni mtoto mchangamfu tangu alipokuwa shule ya msingi.

“Siku moja, nilisikia kuwa amechaguliwa kuwa katibu wa shirika la uongozi wa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Moi, nilifurahi kwa sababu nilijua alipenda uongozi na ndipo safari yake ya kuingia katika siasa ilipoanzia,” akasema.

David anasema kuwa Kindiki amekuwa akitamani kuwa kiongozi kwani alihisi hamu ya kusaidia pale alipoweza na alichaguliwa na wazee alipokuwa bado mdogo kuongoza miradi na vijana wenzake.

Anasimulia kwa mshangao jinsi siku moja walivyomwona kwenye TV huko Hague akiwa na DP Ruto, na kwa hakika walijua kwamba hiyo ndiyo ilikuwa njia yake.

“Pia alituambia kuwa hataki kuwa seneta tena kwani uwezo wake ulikuwa zaidi ya kiti cha useneta,” akasema.

Ruto anatarajiwa kutambulisha mgombea mwenza wake siku ya Jumamosi.