Kigame amteua Irene Ngendo kuwa mgombea mwenza wake

Muhtasari
  • Kigame amteua Irene Ngendo kuwa mgombea mwenza wake

Mwaniaji urais Reuben Kigame ambaye anawania urais kama mgombea huru amemtambulisha Irene Ngendo Kamau kama mgombea mwenza wake kabla ya uchaguzi wa Agosti.

Kigame, mwimbaji wa nyimbo za Injili, alisema ana imani ataibadilisha nchi iwapo atachaguliwa kuwa Rais.

“Mimi na Irene tunaamini katika raia wa nchi hii. Tunaamini kuwa Wakenya wanastahili zaidi ya yale ambayo tumekuwa tukipata,” akasema.

Kigame anasema kuwa lengo lao ni kujenga Kenya kwa kuwawezesha wanawake na wanaume na kupata mustakabali wa watoto.

Kagame ameshikilia kuwa atahakikisha Wakenya hawafukiwi kutokana na matumizi makubwa ya serikali ambayo yanasababisha gharama kubwa ya maisha iwapo atachaguliwa mwezi Agosti. .