Mimi ni bora kuliko wapinzani wangu wote-Babu Owino asema baada ya kuidhinishwa na IEBC

Muhtasari
  • Mbunge huyo aliyezungumza waziwazi ameishukuru IEBC kwa kumpa fursa ya kuchaguliwa tena kwa tiketi ya chama cha ODM
Image: BABU OWINO/TWITTER

IEBC iko katika harakati ya kuwaidhinisha wagombeaji wote kote nchini kabla ya uchaguzi wa Agosti.

Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino ameidhinishwa na tume ya uchaguzi kuwania kiti cha ubunge kwa mara ya pili.

Mbunge Babu Owino alishinda kiti hicho katika kura za 2017 kwa tikiti ya chama cha ODM. Alikuwa amewania kiti hicho bila mafanikio katika kura za maoni za 2013.

Mbunge huyo aliyezungumza waziwazi ameishukuru IEBC kwa kumpa fursa ya kuchaguliwa tena kwa tiketi ya chama cha ODM.

Aliahidi kuendelea kuwatumikia wananchi wa jimbo la Embakasi Mashariki.

"IEBCmuhula mwingine wa  Kuchosha Watu Wa Embakasi Mashariki na Kazi" aliandika Babu.

Owino kwenye ukurasa wake rasmi wa twitter. Babu Owino aliwasihi watu wa Embakasi Mashariki kuunga mkono azma yake ya kuchaguliwa tena kwa tiketi ya chama cha ODM.

Aliongeza kuwa uongozi wake ni bora kuliko wa wapinzani wake.

"Mimi ni bora kuliko wapinzani wangu wote katika kazi, akili, elimu na urembo" aliongeza Babu Owino.

Babu Owino anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa aliyekuwa mbunge wa Embakasi Mashariki Francis Muriithi ambaye ana nia ya kunyakua kiti cha ubunge kwa tiketi ya chama cha UDA.

Francis Muriithi alipoteza kiti kwa Babu Owino katika uchaguzi uliokuwa na upinzani mkali wa 2017.