Raila amshinda Ruto kwa umaarufu- Kura ya maoni

Muhtasari

•  Kulingana na kura hiyo ya maoni Raila angepata kura milioni 9.3 na Ruto kura milioni 8.4 ikiwa uchaguzi ungefanyika leo. 

• Hakuna yeyote kati ya wagombea urais hao wawili ambaye angepata kura 50%+1 ili kuafikia kigezo cha kutangazwa mshindi, kulingana na matokeo ya kura ya maoni.

Naibu rais William Ruto na kinara wa ODM Raila Odinga
Naibu rais William Ruto na kinara wa ODM Raila Odinga
Image: STAR

Mgombea urais wa Muungano wa Azimio One Kenya Raila Odinga ndiye mgombea urais maarufu zaidi ikiwa uchaguzi ungefanyika sasa, kura ya maoni ya Infotrak Research and Consulting imesema. 

Utafiti huo uliofanywa katika maeneo bunge yote 290 unaonyesha kuwa asilimia 42 ya waliohojiwa wangempigia kura Raila huku asilimia 38% wakimtaja Naibu wa rais William Ruto kama mgombeaji wanayempendelea.

 Kulingana na kura hiyo ya maoni Raila angepata kura milioni 9.3 na Ruto kura milioni 8.4 ikiwa uchaguzi ungefanyika leo. 

Hakuna yeyote kati ya wagombea urais hao wawili ambaye angepata kura 50%+1 ili kuafikia kigezo cha kutangazwa mshindi, kulingana na matokeo ya kura ya maoni.

Kulingana na matokeo hayo Raila angeongoza katika kaunti 20 huku Ruto akiwa mbele katika kaunti 16.

 Kiwango cha makosa ya utafiti kiikuwa ni +/-1.

Jumla ya wahojiwa 9,000 walishirikishwa kati ya tarehe 23-27 Mei.

 

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO.