Chagua Rais aliye na heshima,' Martha Karua awahimiza Wakenya

Muhtasari
  • Alisisitiza kwamba kiongozi ambaye haonyeshi heshima kwa wale wanaofanya nao kazi hawezi kuheshimu raia wa kawaida
Martha Karua

 Mgombea mwenza wa urais  Azimio La Umoja Martha Karua mnamo Ijumaa aliongoza kampeni za muungano huo katika kaunti za eneo la Mashariki za Makueni na Kitui.

Karua alipigia debe mgombea urais wa Azimio La Umoja Raila Odinga, akiwataka Wakenya kuwapigia kura wagombeaji chini ya mwavuli wa Azimio katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Agosti.

Alisisitiza kwamba kiongozi ambaye haonyeshi heshima kwa wale wanaofanya nao kazi hawezi kuheshimu raia wa kawaida.

“Kama huna heshima kwa wenzako, pia hutawaheshimu wananchi, ukitaka urais, mheshimu rais aliye madarakani... Na haimaanishi kwamba usimkosee bali fanya kwa utaratibu. hiyo ni ya utaratibu na ina msingi,” alisema Karua, ambaye pia ni kiongozi wa Chama cha NARC-Kenya.

Aliongeza:

"Ukichagua viongozi bila heshima, utakuwa umejidhulumu mwenyewe na pia utadharauliwa. Kibaki alikuwa mnyenyekevu lakini uliona matunda ya uongozi wake. "

Kiongozi huyo wa NARC-Kenya alisema kitu pekee ambacho nchi hiyo inahitaji kwa sasa ili kusonga mbele ni uongozi bora, ambao alisema utatolewa na Odinga na yeye mwenyewe.