Wajackoyah amteua mchekeshaji Jaymo Ule Msee kuwa msemaji wake na mkuu wa vyombo vya habari

Muhtasari
  • Wakati akikubali uteuzi huo, Jaymo alisema kuwa ilikuwa heshima kubwa kupata fursa kama hiyo ya kufanya kazi na Wajackoyah
Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Jaymo Ule Msee

Mwaniaji urais wa Chama cha Roots George Wajackoya alishangaza wengi alipojitokeza miongoni mwa wagombea wanne bora wa urais ambao waliidhinishwa kuwania urais katika uchaguzi ujao.

Wakili huyo mkongwe ambaye amekuwa kivutio kufuatia msimamo wake kuhusu bhangi na katiba miongoni mwa mambo mengine, ameendelea kupata umaarufu zaidi kadiri siku zinavyosonga.

Wajackoyah leo amepiga hatua nyingine ambayo imewafanya wakenya kushangazwa na jinsi huyu jamaa anavyofanya mambo yake.

Katika tangazo lake la hivi punde, Wajackoya amemteua mcheshi na mtayarishaji maudhui Jaymo Ule Msee kuwa Msemaji wake na mkuu wa Vyombo vya Habari.

Wakati akikubali uteuzi huo, Jaymo alisema kuwa ilikuwa heshima kubwa kupata fursa kama hiyo ya kufanya kazi na Wajackoyah.

Alikishukuru chama na wote waliofanikisha hili na kuwahakikishia kuwa atafanya kazi bila kuchoka ili kuleta ushindi kwa wajackoyah.

"Ni kwa unyenyekevu mkubwa kwamba ninakubali kuteuliwa kuwa msemaji wa Roots Party & Mkuu wa Vyombo vya Habari. Namshukuru sana tarehe 5 @profgeorgewajackoyah , mgombea mwenza Justina Wamae na viongozi wetu wa chama kwa kuwa na imani nami kutumikia chama chetu ili kuhakikisha tunapata ushindi wa kishindo tarehe 9 Agosti .Ni wakati wa kizazi chetu kufanya maamuzi sahihi."