logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Khalwale apigwa mawe baada ya kukosa kumuidhinisha Malala kuwania ugavana Kakamega

Alijipigia debe huku akijigamba kuwa yeye ndiye mtunzi sheria bora anayejulikana kote nchini.

image
na SAMUEL MAINA

Uchaguzi15 June 2022 - 03:30

Muhtasari


  • •Tukio la mtafaruku lilizuka na kupelekea gari lake kutupiwa mawe alipokuwa akikimbia kwa kasi kuokoa maisha yake.
  • •Aliwataka wakazi kuwapima viongozi wote kutoka eneo hilo na kumchagua yeyote wanayemtaka kwa wadhifa wowote.
Boni Khalwale wakati wa uchaguzi katika eneo Bunge la Kbra

Aliyekuwa seneta wa Kakamega Boni Khalwale alikumbana na ghadhabu ya wakazi katika eneo la Matungu, kaunti ya Kakamega.

Tukio la mtafaruku lilizuka na kupelekea gari lake kutupiwa mawe alipokuwa akikimbia kwa kasi kuokoa maisha yake.

Masabu yalianza baada yake kukosa kumuidhinisha Seneta Cleophas Malala kuwania kiti cha ugavana licha ya wote wawili kuwa katika Muungano wa Kenya Kwanza.

Seneta huyo wa Zamani aliwataka wakazi kuwapima viongozi wote kutoka eneo hilo na kumchagua yeyote wanayemtaka kwa wadhifa wowote.

Hata hivyo, alijipigia debe huku akijigamba kuwa yeye ndiye mtunzi sheria bora anayejulikana kote nchini.

"Sote tunatafuta viti. Tupimeni na mmchague yeyote ambaye mnamtaka kwa kiti chochote. Chagua atakayekujali. Kumbuka Khalwale ndiye mtunzi sheria bora nchini Kenya."

Matamshi hayo yalimzonga Malala ambaye alikabiliana naye uso kwa uso akisema "amechanganyikiwa".

Ni baada ya makabiliano hayo ambapo Khalwale alilazimishwa kutoroka mkutano huo na  wafuasi wa Malala waliokuwa wamejawa na hasira.

"Ondoka hapa. Toweka," seneta huyo aliamrishwa na vijana wenye ghasia kwenye video iliyofikia Radio Jambo.

Huku walinzi wake wa usalama wakisafisha njia, kundi lililokuwa na ghadhabu lilifuata gari lake likimwambia aharakishe.

Mambo yalizidi kuwa mabaya baada ya kundi hilo kuanza kurusha mawe kuelekeza kwenye msafara wake.

Hatimaye seneta huyo alifanikiwa kuondoka katika eneo hilo la ghassia huku vijana hao wakiendelea kurushia mawe gari lake.

Baada yake kuondoka eneo la tukio, vijana hao walisikika wakiimba: "Tunamtaka Lishenga! Tunataka lishenga!"

Lishenga ndiye mgombeaji wa ODM kwa kiti cha useneta wa Kakamega.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved