Mashirika ya kijamii ya Kisii kuandaa midahalo ya wagombea ugavana

Muhtasari

•Mashirika ya kijamii mjini Kisii yameandaa mdahalo wa wagombeaji wa kiti cha ugavana

•Bali na kukata tamaa Wakenya  pia wamechoka kutokana na gharama ya juu ya maisha.

•Idara ya kudhibiti gharama za Mafuta na Kawi imeshindwa kufanya kazi yao.

Mwaniaji wa ugavana wa Kisii Simba Arati wakati wa kikao na wanahabari katika afisi ya eneo la Azimio mjini Kisumu Jumamosi. Picha: MAURICE ALAL
Mwaniaji wa ugavana wa Kisii Simba Arati wakati wa kikao na wanahabari katika afisi ya eneo la Azimio mjini Kisumu Jumamosi. Picha: MAURICE ALAL
Image: MAURICE ALAL

Mashirika ya kijamii mjini Kisii yameandaa mdahalo wa wagombeaji wa kiti cha ugavana katika Kaunti hiyo.

Mjadala huo utakaoandaliwa katika Chuo Kikuu cha Kisii mnamo Julai 7 unasemekana kuwapa nafasi ya kuuza manifesto na ajenda zao kwa wakazi wa Kisii.

Mashirika hayo yamechukizwa na ukiukwaji wa sheria na kanuni za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) na wagombeaji wa viti maalum, wakitaja kuwa ni makosa na kutokubalika.

Waliongozwa na John Omangi, Askofu wa Kanisa la Anglikana Kenya (ACK), Dayosisi ya Nyanza Kusini.

Omangi aliwataka wagombeaji wote kuzingatia kanuni za IEBC zinazowataka kuanza kampeni zao ifikapo saa sita asubuhi na kumalizikia saa sita jioni, akibainisha kuwa wagombeaji wanafanya kampeni usiku na kuwasumbua wakazi.

Kwa wakati huo  wito ulitolewa kwa IEBC na wasimamizi wa sheria kufuatilia kampeni na kuchukua hatua dhidi ya wagombea, na wafuasi wao ili kupunguza ghasia.

“Kampeni za usiku zinatuathiri. Hatuwezi kulala. Mwenendo huo ni mbaya na ninawaomba wanasiasa wakomeshe na kuzingatia kanuni za maadili walizotia saini walipoidhinishwa na bodi ya uchaguzi,” askofu Omangi aliambia wanahabari.

Akizungumza baada ya ibada katika kanisa la Mtakatifu Philip ACK katika makao makuu, Askofu huyo, akiwa na vijana na wanawake wa kanisa hilo, alisema kuwa tangu kampeni zilipoanza, utoaji wa huduma umekuwa duni katika kaunti hiyo.

Alisema Baadhi ya watumishi wa umma wameacha majukumu yao na kuwaacha Wakenya wakiteseka kutokana na gharama ya juu ya mafuta, mafuta ya kupikia na unga kote nchini.

Bali na kukata tamaa, Wakenya  pia wamechoka kutokana na gharama ya juu ya maisha.

Omangi alisema Mamlaka ya kudhibiti  Nishati na Petroli, iliyopewa jukumu la kudhibiti bei ya mafuta na gesi haijawahi kupunguza bei yake na kuitaka serikali kuingilia kati na kuwaepusha Wakenya dhidi ya kupanda kwa gharama ya maisha.

Serikali inafaa kuhakikisha kuwa Wakenya wana chakula cha kutosha. Je, inamaanisha kuwa hakuna chakula katika Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao (NCPD) ili kupunguza mateso ya Wakenya maskini?" alisema

Omangi alibainisha kuwa wengi wa Wakristo maskini walikuwa wakiomba chakula kutoka kwa viongozi wa makanisa na akaomba serikali kuingilia kati na kupunguza bei ya vyakula ili kuimarisha maisha ya Wakenya.