Raila ndiye mgombea urais maarufu zaidi Nairobi- Kura ya maoni

Muhtasari

•Mgombea urais wa Azimio la Umoja Raila Odinga ndiye mgombea urais anayependelewa zaidi jijini Nairobi, Tifa Research imesema.

•Kura ya maoni ilifanyika Juni 20, 2022 ambapo wahojiwa 632 ambao wote ni wapiga kura waliojiandikisha walihojiwa.

Raila Odinga
Mgombea urais Raila Odinga Raila Odinga
Image: RAILA ODINGA/TWITTER

Mgombea urais wa Azimio la Umoja Raila Odinga ndiye mgombea urais anayependelewa zaidi jijini Nairobi, kura ya maoni ya TIFA imesema.

Katika matokeo ya kura zilizotolewa Jumanne, Raila anaongoza Nairobi kwa asilimia 50 huku Naibu Rais William Ruto akimfuata kwa asilimia 25.

George Wajackoyah wa Roots Party anaibuka wa tatu kwa asilimia 7.

Hata hivyo, asilimia 18 ya waliohojiwa bado hawajaamua ni nani wa kumpigia kura.

Kura hiyo ya maoni inaonyesha ongezeko la asilimia tisa kwa upande wa Raila ikilinganishwa na Mei ambapo aliongoza kwa asilimia 41.

Upande wa Ruto ulionyesha kushuka kwa asilimia moja ikilinganishwa na Mei alipokuwa na asilimia 26.

Kura ya maoni ilifanyika Juni 20, 2022 ambapo wahojiwa 632 ambao wote ni wapiga kura waliojiandikisha walihojiwa.

Mahojiano hayo yalifanyika kwa njia ya simu.

Kura ya maoni ina hitilafu ya ukingo ya asilimia +/-3.8.

Seneta wa Nairobi Johnson Sakaja ambaye ni mgombeaji wa United Democratic Alliance (UDA) bado ndiye mgombea anayependekezwa zaidi wa kiti cha ugavana wa Nairobi, huku asilimia 40 ya waliohojiwa wakiunga mkono azma yake.

Anafuatwa kwa karibu na Azimio la Umoja Polycarp Igathe kwa asilimia 32.