Afueni kwa Sonko baada ya mahakama kusimamisha uchapishaji wa karatasi za kura katika kinyang'anyiro cha ugavana

Muhtasari
  • Afueni kwa Sonko baada ya mahakama kusimamisha uchapishaji wa karatasi za kura katika kinyang'anyiro cha ugavana
Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko
Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko
Image: Facebook// Mike Sonko

 Mahakama kuu iliyoko Mombasa imetoa amri ya muda ya kuzuwia IEBC kuchapisha karatasi za kupigia kura za kinyang'anyiro cha ugavana Mombasa, ikisubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa ombi lililowasilishwa na aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko. .

Benchi la majaji watatu pia lilitoa maagizo ya kihafidhina kusimamisha baraza la uchaguzi kutangaza majina ya wagombeaji katika kinyang'anyiro cha ugavana Mombasa.

Majaji hao ni pamoja na;jaji Olga Sewe, Ann Ong'injo' na S. Githinji walisimamisha Chama cha Wiper kuteua mgombeaji mwingine kusubiri kusikilizwa kwa ombi hilo.

Sonko anataka kubatilisha uamuzi wa Kamati ya IEBC ya Kusuluhisha Mizozo ya kumzuia kuwania kiti cha Ugavana wa Mombasa.

Kesi itaendelea saa nane.