Mjadala wa urais kufanyika Julai 26

Muhtasari
  • Katika taarifa ya Jumatatu, sekretarieti hiyo pia ilisema mjadala wa naibu rais utafanyika Jumanne, Julai 19
Image: KWA HISANI

Mjadala wa urais 2022 utafanyika Julai 26, Mkuu wa Sekretarieti ya Mijadala ya Rais Clifford Machoka amesema.

Katika taarifa ya Jumatatu, sekretarieti hiyo pia ilisema mjadala wa naibu rais utafanyika Jumanne, Julai 19.

Sekretarieti hiyo pia imeandaa mijadala ya wagombeaji ugavana wa Nairobi ambayo itaandaliwa Jumatatu, Julai 11.

Mijadala yote itafanyika katika chuo kikuu cha Catholic University for Eastern Africa (CUEA) kilichoko Karen, Nairobi, kuanzia  saa kumi na moja jioni hadi nne usiku.