"Rais Kenyatta alikuwa mtu wa kusitasita bila maamuzi" Kindiki, Kositany waelezea

Caleb Kositany na Profesa Kindiki katika hafla tofauti walielezea kwamba Uhuru Kenyatta ni mtu ambaye lazima alazximishwe kufanya jambo

Muhtasari

• Kositany alieleza kwamba wakati Moi alimtaka Uhuru kujitosa siasana, alikataa ikabidi kina Kositany waongee na yeye hadi akakubali.

• Kwa upande wake profesa Kindiki alieleza 2013 walimlazimisha Kenyatta kuwania urais na yeye ndiye alichana makubaliano ya kupeana nafasi hiyo kwa mtu mwingine.

• Viongozi hao walikuwa wakizungumza kumtetea Ruto kwamba alimlazximisha Kenyatta kuwania urais wa marudio ya uchaguzi, mpaka karibu kumzaba kofi.

Mbunge wa Soy, rais Uhuru Kenyatta na seneta wa Tharaka Nithi
Caleb Kositany, Uhuru kenyatta, Kithure Kindiki Mbunge wa Soy, rais Uhuru Kenyatta na seneta wa Tharaka Nithi
Image: Twitter, State House Kenya

Baadhi ya viongozi mbalimbali wamejitokeza kudhihirisha wazi dhana ambayo imekuwa ikizungumzwa sana kwamba naibu rais William Ruto ni mtu mwenye misimamo mikali isiyoteteleka kulinganishwa na rais Kenyatta ambaye ni mwepesi wa kufa moyo katika kufanya kitu.

Tukimzungumzia rais Kenyatta kwa mapana kwa kuangazia dhana kwamba kiongozi huyo wa Jubilee ni mwepesi sana kuachia kitu anachokitaka maishani, mbunge wa Soy Caleb Kositany ameeleza kwamba amemjua rais kuwa ni mtu mwenye kufa moyo haraka mno.

Akirudisha Wakenya nyumba kabisa wakati rais Kenyatta alikuwa anajitosa rasmi kwenye siasa enzi za uongozi wa hayati Daniel Moi, Kositany anaeleza kwamba Moi alijaribu kumuambia Kenyatta lakini akaona kama hajaridhia na hivyo kutumia baadhi ya watu kumshawishi.

“Mimi nimekuwa Rafiki wa Uhuru kabla hata hajaingia siasa. Na wakati hayati rais Moi alimueleza Uhuru nataka uingie katika kiwanja cha siasa, mimi nilikuwa nimesimama hapo tukiwa katika ikulu na Uhuru Kenyatta. Na Uhuru alikataa kabisa kuingia mambo ya siasa. Na rais Moi alipokuwa akiondoka akaniambia Caleb eleza yeye,” Kositany aliibua kumbukumbu katika mahojiano na runinga moja nchini.

Mbunge huyo alikuwa akitolea mfano kwamba rais Kenyatta si mtu wa kufanya jambo pasi na kusukumwa na watu wenye misimamo mikali, katika kile kilionekana kwamba anamtetea Ruto kwacmadai ya kutaka kumpiga kofi Kenyatta alipokataa kuwania uchaguzi wa marudio 2017.

Kositany pia alielezea hali hiyo ilijitokeza mwaka 2013 ambapo walikuwa wanatafuta mpeperusha bendera wa urais kati ya Kenyatta, Ruto na Mudavadi, ambapo Uhuru alitaka wamuunge mkono Mudavadi na wao waliketi chini wakamshawishi mpaka akakubali kuwa mpeperusha bendera, jambo lililomfanya Mudavadi kugura muungano huo na kugombea kivyake.

Naye seneta wa Tharaka Nithi, msomi profesa Kithure Kindikialimwaga mtama kwambamwaka wa 2013 Uhuru alikuwa ashakubali mkataba wa kumuunga Mudavadi mkono lakini walimlazimisha.

“Acha niwaambie ukweli, Uhuru Kenyatta alikuwa mgombea wa kusitasita. Mimi mwenyewe 2013 nilikuwa wakili wa Uhuru na William Ruto. Wakati ilisemekana kwamba Ruto na Kenyatta wangepatana na vikwazo vingi kutoka jamii ya kimataifa kutokana na kesi yao ya ICC, Kenyatta alitia mkataba haramu wa kubadilisha upeperushaji bendera kwenda kwa Mudavadi, mimi nilichana karatasi ya huo mkataba na tukamwambia ni yeye atawania,” Profesa Kindiki alisema.