Tazama: Wagombea wa ugavana Nairobi wamenyana kwenye mdahalo

Wagombea tisa wameidhinishwa kuwania kiti cha ugavana wa Nairobi

Muhtasari

•Wagombea tisa wameidhinishwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka kuwania kiti cha ugavana wa Nairobi mnamo Agosti 9, 2022.

Wagombea tisa wameidhinishwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka kuwania kiti cha ugavana wa Nairobi mnamo Agosti 9, 2022.

Johnstone Sakaja wa UDA, Polycarp Igathe wa Jubilee, Agnes Kagure, Nancy Wambui Mwandime, Kenneth Nyamwamu, Cleophas Kiio Mutua, Harman Singh Grewal, Esther Waringa Thairu na Denise Kodhe ndio watakaopimana nguvu katika kinyang'anyiro cha ugavana wa Nairobi mwezi ujao.

Wagombea hao wanatarajiwa kushiriki mdahalo ambao umepangwa kufanyika jioni ya Jumatatu.

Wanahabari wanne waliochaguliwa na Sekretarieti ya Mdahalo wa Urais watasimamia mdahalo huo utakaofanyika katika kampasi kuu ya Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki (CUEA) huko Karen, Nairobi.

Mjadala huo utakaoonyeshwa kwenye televisheni unakuja wiki moja tu kabla ya mjadala wa wagombea wenza wa kiti cha urais ambao utafanyika mnamo Julai 19 na wiki mbili kabla ya mdahalo wa urais utakaofanyika Julai 26.