Nitafanya kazi yangu hadi dakika ya mwisho-Uhuru kwa wakosoaji wake

"Hawa wengine ni wa mdomo tu na matusi. Ukiwaona wanakutana wananizungumzia mimi," alisema.

Muhtasari
  • Uhuru pia aliunga mkono mgombeaji urais wa Azimio Raila Odinga akisema ndiye mtu bora zaidi kumrithi
Rais Uhuru Kenyatta
Image: PSCU

Rais Uhuru Kenyatta amemsuta naibu wake William Ruto kuhusu matamshi kwamba anafaa kuzingatia tu kustaafu kwake kabla ya uchaguzi wa Agosti 9, mwaka huu.

Uhuru ambaye alikuwa akizungumza jijini Nairobi alipozindua miradi alisema haendi popote hadi amalize kazi yake.

"Hawa wengine ni wa mdomo tu na matusi. Ukiwaona wanakutana wananizungumzia mimi," alisema.

"Sitafuti kura. Wananiambia nimalizie niende, wanataka niende wapi? Nitafanya kazi yangu hadi dakika ya mwisho."

Uhuru alisema bado ana kazi nyingi anazofanya na hatakwenda hadi amalize zote.

Uhuru pia aliunga mkono mgombeaji urais wa Azimio Raila Odinga akisema ndiye mtu bora zaidi kumrithi.

"Bado kuna kazi nyingi za mawazo. Hospitali zinafaa kufunguliwa.. Nitazifanya mpaka nimpe rais ajaye na naomba mtu ambaye nitampitishia rungu. Raila Odinga," alisema.