Mbilia Bel: Nitaimba na kucheza densi kwenye kampeni mpaka Raila ashinde

Wikendi iliyopita mwanamuziki huyo alionekana kwenye video akimchezesha densi Raila Odinga jukwaani wakati wa hafla ya kampeni.

Muhtasari

• Mwanamuziki huyo mkongwe alisema alimchagua Raila kwa sababu ndiye alizungumza na moyo wajke.

• Alisema anampigia debe Raila kwa sababu aliguswa na kitendo chake cha kuchagua mwanamke kama mgombea mwenza.

Mwanasiasa Raila Odinga akichezaq densi na mwanamuziki Mbilia Bel
Mwanasiasa Raila Odinga akichezaq densi na mwanamuziki Mbilia Bel
Image: YouTube (Screengrabs)

Mwanamuziki mkongwe wa mtindo wa rhumba kutokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mbilia Bel ameweka wazi kwamba hakulipwa ili kutumbuiza katika hafla ya kinara wa Azimio-One Kenya, Raila Odinga.

Malkia huyo wa muziki alifichua kwamba alipenda tu sera za Raila haswa kwa kitendo cha kumteua mwanamke(Martha Karua) kuwa mgombea mwenza na hilo litamfanya aimbie Raila mpaka pale atakapoapishwa kama rais wa tano wa Kenya.

Katika mahojiano ya kipekee na gazeti moja humu nchini, Bel alisema kwamba anamheshimu sana Raila Odinga na mgombea mwenza kwa sababu wao ni kama wqazazi kwetu.

“Niko hapa kwa kujitolea tu na pia kwa mapenzi yangu kwa Raila Odinga na mgombea mwenza wake. Nitaimba mpaka Odinga awe rais mnamo Agosti 9. Ninampigia upato kwa sababu manifesto yake na ile handshake na rais Kenyatta viliunganisha nchi,” Bel alitetea uamuzi wake wa kutumbuiza katika hafla za Raila.

Mwanamuziki huyo ambaye alitua nchini wiki jana alisema kwamba Kenya ni kama nchi yake ya pili na kila mara anapoalikwa kuja kutumbuiza huwa anajihisi kuheshimika sana.

Pia Bel alisema hana chuki na Ruto ila tu ameamua kumpigia upato Raila na kusema kwamba mwanasiasa huyo mkongwe kila mara ako Kongo anawasaidia kuhubiri amani.

“Msisahau kwamba William Ruto pia ni Mkenya lakini mimi nilimchagua Raila kwa sababu yeye alizungumza na moyo wake na yeye huwa anahubiri amani na umoja kwa watu wa Afrika, ndio maana nampigia upato bwana Raila kupitia muziki wangu,” alisema Bel.

Wikendi iliyopita, Bel alionekana jukwaani akimuimbia na kumchezesha kinara wa Azimio-One Kenya, Raila Odinga katika moja ya densi zilizozungumziwa sana haswa kwenye mitandao ya kijamii.