Ruto sasa atahudhuria mjadala wa urais

Viongozi wa UDA wamethibitisha kuhudhuria kwake

Muhtasari

•Kulikuwa na shaka juu ya mahudhurio yake baada ya baadhi wa  viongozi wake kumshauru asihudhurie mjadala kupinga kile walichokiita "upendeleo wa vyombo vya habari".


Viongozi wa kampeni ya Naibu Rais William Ruto wakihutubia kongamano Alhamisi, Julai 21, 2022.
Viongozi wa kampeni ya Naibu Rais William Ruto wakihutubia kongamano Alhamisi, Julai 21, 2022.
Image: STAR

Naibu Rais William Ruto atahudhuria mdahalo wa urais ulioratibiwa Jumanne, Julai 26.

Hussein Mohamed, anayesimamia mawasiliano ya Ruto, alithibitisha kuhudhuria kwake.

Pia ametoa masharti kwa waandalizi akiwataka kuweka hadharani muda uliotengwa kwa ajili ya watahiniwa hao kujieleza kuhusu mipango yao kwa Wakenya.

Alipinga namna mdahalo wa naibu rais ulivyoendeshwa akisema licha ya mamilioni ya watu kutazama, hakuna masuala ya mada  muhimu yaliyoulizwa.

Hussein alisema waliohoji badala yake walipuuza mjadala kwa kujadili watu binafsi na uhusiano wa kisiasa.

“Ingawa hatupingi maswali yanayoulizwa katika mijadala hiyo, tunapinga kukosekana kwa baadhi ya vitu muhimu zinazo sumbua  Wakenya,” akasema.

Katibu wa kidijitali wa Ruto Dennis Itumbi alisema Naibu Rais amesisitiza kutengwa kwa muda maalum kwa masuala kadhaa.

Alitaja elimu, uchumi,afya, elimu, uchumi wa kidijitali na ubunifu, miongoni mwa mambo mengine, kuwa ni baadhi ya maeneo ambayo anataka wasimamizi kutaja muda  wakujibu swali.

Wagombeaji wa Urais  wengine ambao pia watakuwa kwenye mdahalo huyo ni pamoja na Raila Odinga wa Azimio one Kenya, George Wajackoyah wa Roots party of Kenya na David Mwaure wa Agano party.

Wakenya wengi wanatazamia kusikiza kile watakao sema wakati wa mdahalo huo, ili kufanya uamuzi mwafaka kwa yule watakao mpigia  kura mnamo Agosti 9.

Mhadalo ya wangombeaji wenza ulifanyika Jumanne ambayo ulihusisha manaibu wote kutoka kwa mirengo hizo za kisiasa.

 

Viongozi wa kampeni ya Naibu Rais William Ruto wakihutubia kongamano Alhamisi, Julai 21, 2022.
Viongozi wa kampeni ya Naibu Rais William Ruto wakihutubia kongamano Alhamisi, Julai 21, 2022.
Image: STAR