"Ruto ananishinda tu kwa miaka na wizi, ana digrii moja mimi nina nne" - Babu Owino

Babu Owino alisema maandalizi yake dhidi ya Ruto katika mdahalo wa urais yanapamba moto.

Muhtasari

• Babu Owino - Ruto ananishinda tu kwa miaka na wizi.

Mbunge Babu Owino akijiiandaa kwa mdahalo dhidi ya William Ruto.
Mbunge Babu Owino akijiiandaa kwa mdahalo dhidi ya William Ruto.
Image: Facebook//BabuOwino

Baada ya mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed kufanya mzaha kwamba muungano wa Azimio la Umoja One Kenya utamtuma mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino kumenyana na mpeperusha bendera wa Kenya Kwanza William Ruto kwenye mdahalo wa urais, sasa ni kama Babu Owino alichukulia utani ule kiuhakika na ameendeleza msururu wa vituko vyake mitandaoni akisema ni kujiandaa kwa ajili ya mdahalo huo dhidi ya naibu rais William Ruto.

Wikendi iliyopita, Owino alipakia picha na video kadhaa, alisema kwamab anajiandaa kupambana na Ruto kwa ukakamavu kubwa, jambo ambalo wiki jana alisema kwamba ako tayari kushiriki kwa niaba ya Raila kwa sharti kwamba Ruto alizungumzie masuala ya toroli na uongo mbele yake, akijiita msomi.

“Niko tayari kushiriki mdahalo na Ruto kwa sharti kwamba hatasema uongo na hatataja neno toroli mbele ya msomi. Nitampeleka kwenye Usahaulifu wa kisiasa ambao ni kuzikwa kwa wasiostahili kwenye mavumbi yao ya utupu,” alisema Owino.

Suala hili la kujiita msomi na kumdunisha Ruto liliwachukiza baadhi ya wafuasi wa Ruto ambao walimuambia kwamba naibu rais si kiwango chake na hafai katu kujilinganisha naye, Owino alijibu kwa kusema kwamba Ruto kitu anachomshinda ni umri na wizi tu na si mengine.

“Ruto sio kiwango chako, kwa kweli tutamtuma mbunge Oscar Sudi kunyamazisha midomo yako,” mmoja kwa jina Joe Losif alimwambia Owino kulingana na picha ambayo mbunge huo alipakia kwenye Ukurasa wake wa Facebook.

“Nina shahada nne na astashahada sita na Ruto ana shahada moja. Nilisoma Acturial Science na kupata alama katika kipengee cha kwanza, nikafanya sheria na nikapita kwac daraja la pili, hali ya kuwa Ruto alisoma mimea na kufuzu kwa kipengee cha pili daraja la chini,” Babu Owino alitanua kifua.

Wikendi, kamati ya kusimamia kampeni za Raila kupitia msemaji wake profesa Makau Mutua walisema kwamba wameafikia uamuzi wa kumkataza Raila kutohudhuria mdahalo huo kwa kile walisema kwamba hadhi yake haimruhusu kushiriki meza moja ya mdahalo na naibu rais William Ruto.