"Hadithi yangu inahamasisha kila mtu kuinuka na kuangaza, kujikwaa na kuinuka" - Fatuma Jehow

Mwanasiasa huyo alisema haya baada ya kutembelea nyumba walimokuwa wakiishi wakati baba yao alikuwa chifu eneo hilo.

Muhtasari

• "Hadithi yangu inawahusu mayatima wote na Wajir wengi,” alisema Fatuma Jehow.

• Alisema kufika katika nyumba hiyo kuliibua kumbukumbu nzito ambazo alisema akiwa mwakilishi wa kike atafanay kweli kurudisha mkono kweye jamii nzima iliyomlea.

Mwanasiasa anayelenga kuwa mwakilishi wa kike kaunti ya Wajir, Fatuma Abdi Jehow
Mwanasiasa anayelenga kuwa mwakilishi wa kike kaunti ya Wajir, Fatuma Abdi Jehow
Image: Facebook//FatumaAbdiJehow

Fatuma Jehow, mwanasiasa anayelenga kuwa mwakilishi wa kike katika kaunti ya jangwani ya Wajiri kaskazini mashariki mwa Kenya kupitia tikiti ya chama cha ODM amegusa mioyo ya wengi baada ya kupakia picha ya nyumba mbovu ambayo alisema ndio yalikuwa makaazi yao miaka ya nyuma.

Mwanasiasa huyo alijawa na kumbukumbu nyingi huku akisema kwambaq kasri hilo jeupe lilikuwa makaazi yao wakati baba yao marehemu alikuwa anahudumu kama mkuu mwanzilishi wa kata ya Wajir-Bor.

Mwanasiasa huyo alisema kurejea pale kuliibua kumbukumbu nzito ambazo alisema kwa upande wake kuona jumba lile kunamchorea kichwani taswira ya mayatima maskini, haswa wale wanaoishi kwenye kaunti hiyo yenye shida si haba.

“Nyumba nyeupe nyuma yangu ilikuwa nyumba yetu duni wakati marehemu baba yetu alihudumu kama mmoja wa machifu waanzilishi huko Wajir-Bor na viunga vyake. Sote tuna hadithi ya kusimulia, Hadithi yangu inawahusu mayatima wote na Wajir wengi,” alisema Fatuma Jehow.

Katika kile kilionekana kama njia moja ya kujipigia kampeni, Jehow alisema kwamba kumbukumbu hizo nzito zinamtanda kichwani na ndio maana uongozi wake kama mwakilishi wa kike umelipa suala hilo kipaumbele, ili kila mtu awe na nafasi ya kuinuka na kuangaza kutoka uhayawinde wa aina hiyo.

“Kwa hivyo, hadithi yangu sio tofauti, lakini kugombea kwangu pia ni kuhamasisha kila mtu, kuinuka na kuangaza, kujikwaa na kuinuka, kupokea na kurudisha kwa jamii bila kujali ni ndogo na zaidi ya yote kutumikia nafasi ya uongozi. Wakati wangu utakapofika, ni sasa na niko tayari zaidi,” Fatuma Jehow alisema kwa kumbukumbu zenye hisia nzito kama nana.

“Maisha yako ya nyuma na hali yako kama ilivyo sasa na azimio na bidii ya kuwatumikia na kuwainua waliokandamizwa na walio wachache ndio inafafanua na kuitwa EPOCH ya ajabu,” mmoja kwa jina Musa Wayax alimpongeza.

I was filled with emotions yesterday when I visited our house in Wajir-Bor where my siblings were born and partially...

Posted by Hon Fatuma Abdi Jehow For Women Rep 2022 on Monday, July 25, 2022