Msimchague mwizi kuwa rais,'Uhuru kwa Wakenya

Uhuru aliendelea kusema kuwa kazi ambayo amefanya katika kipindi cha miaka kumi ya uongozi ni dhahiri.

Muhtasari
  • Rais Uhuru Kenyatta amewataka Wakenya kuwa waangalifu wasimchague kiongozi asiyejali maslahi ya nchi moyoni
Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta
Image: PSCU

Rais Uhuru Kenyatta amewataka Wakenya kuwa waangalifu wasimchague kiongozi asiyejali maslahi ya nchi moyoni.

Uhuru alisema Wakenya hawafai kung'ang'ania dakika za mwisho na kuharibu kile ambacho eneo hilo limejenga kwa miaka mingi hivyo hawafai kupiga kura ya kijambazi.

Akizungumza alipokuwa akizindua bwawa huko Gatundu Kaskazini, Kaunti ya Kiambu, aliomba eneo hilo kutosikiliza kile ambacho amewaahidi, akitaja kuwa maneno matupu.

“Jizuieni msichague mwizi, sitaki kusikia mnalia kujuta, kuna watu wana hadithi za kuchekesha lakini ni tamu kama asali na zinashawishi, lakini ni sumu,” alisema.

Uhuru aliwataka vijana ambao ni viongozi wa kesho, kujua wanachotaka na ni nini cha msaada kwao na nini kitabadilisha nchi.

"Vijana tutawaachia nchi hii, jiulizeni mmeona nchi imegeuzwa mikokoteni, mnataka mikokoteni au njia za kuwapeleka watoto shuleni? ukitaka kusukuma mikokoteni ni sawa, " alisema.

Uhuru aliendelea kusema kuwa kazi ambayo amefanya katika kipindi cha miaka kumi ya uongozi ni dhahiri.

Alisema wanaosema hajafanya kazi waangalie miradi aliyoianzisha na kuiendeleza.

"Kuna watu wanajua matusi tu, badala ya sisi kujumuika na kufanya kazi na kuleta amani, wamekuwa wakisema hakuna kazi, hili bwawa limejijenga lenyewe? barabara zilijenga zenyewe?hata pale ambapo watu walidhani umeme hautafika, ulifika, ulienda wenyewe huko?aliuliza.

Kisha akaunga mkono mgombea mwenza wa urais wa Azimio Raila Odinga na mgombea mwenza wake Martha Kar