Mama wa kambo wa Malala agura Kenya Kwanza, awaidhinisha Raila na Barasa

Barasa wa ODM anawania kiti cha ugavana dhidi ya Malala ambaye anawania kwa tiketi ya ANC

Muhtasari
  • Akizungumza wakati wa mkutano huo, Raila aliahidi kufufua shughuli za Kampuni ya Sukari ya Mumias
Image: Wycliffe Oparanya/FACEBOOK

Mamake wa kambo wa Seneta wa Kaunti ya Kakamega Cleophas Malala amgura Kenya Kwanza kwa Azimio.

Jackeline Okanya alitangaza kuunga mkono ombi la Raila Odinga wakati wa mkutano wa Azimio katika uwanja wa Bukhungu siku ya Jumatano.

"Nimetoka Kenya Kanza. Nimekuja Azimio kusaidia Baba na Martha. Nimekuja kusaidia gavana wangu Barasa na Savula ili Kenya yetu iweze kwenda mbele,"Alizungumza Okanya.

Okanya anawania kiti cha ubunge cha Mumias Magharibi, ambapo alimhakikishia Raila kwamba eneo hilo litaongozwa na viongozi washirika wa Azimio.

Anagombea kwa tiketi ya ANC. Mnamo Juni 19, aliombwa kuachia ngazi kwa ajili ya Rashid Echesa wa UDA, jambo ambalo alilikanusha.

Barasa wa ODM anawania kiti cha ugavana dhidi ya Malala ambaye anawania kwa tiketi ya ANC, Cyrus Jirongo (UDP), na Samuel Omukoko wa Maendeleo Democratic Party (MDP) miongoni mwa wengine.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Raila aliahidi kufufua shughuli za Kampuni ya Sukari ya Mumias.