Jalang'o ajiamini kushinda kinyang'anyiro cha ubunge Lang'ata

Jalang'o alipiga kura katika shule ya msingi ya Uhuru Gardens mapema asubuhi.

Muhtasari

•Jalang'o alionyesha imani kuwa atawashinda wapinzani wake katika kinyang'anyiro hicho na kuapishwa kama mbuge wa Langata.

Jalango
Jalango
Image: Hisani

Mtangazaji aliyegeuka kuwa mwanasiasa Felix Odiwuor, almaarufu Jalang'o amehutubia wafuasi wake baada ya kujipigia kura.

Mgombea ubunge huyo wa Lang'ata kwa tikiti ya ODM alipiga kura katika shule ya msingi ya Uhuru Gardens mapema asubuhi.

Jalang'o alionyesha imani kuwa atawashinda wapinzani wake katika kinyang'anyiro hicho na kuapishwa kama mbuge wa Langata.

Pia alisema kuwa atatembelea vituo vingine vya kupigia kura ndani ya jimbo hilo ili kuhakikisha wafuasi na maajenti wake wako salama.

''Lazima nitembee niakikishe kwamba agents wangu wako vizuri an taratibu zote zinafuatwa ili kusiwe na hitilafu yeyote. Sisi tuko tayari kufanya kazi na kuhakikisha kwamba tumemaliza vizuri," Alisema.

Mtangazaji huyo wa zamani wa redio pia aliwashukuru mashabiki wake kwa kumuunga mkono hadi mwisho wa safari.

"Tumepiga kura an nimamaliza. Asanteni sana kwa ambao wamekuwa nasi katika hii safari. Haijkuwa safari rahisi, imekuwa safari ndefu na tumemaliza sasa ni kusubiri tu an kuona kuwa tunapata mafanikio," Jalang'o aliongeza.