Jamaa akamatwa baada ya kupatikana na panga na kisu katika kituo cha kupigia kura Homa Bay

Polisi walimpata mshukiwa walipokuwa wanakagua kituo hicho baada ya shughuli za upigaji kura kukamilika.

Muhtasari

•Mshukiwa alikamatwa Jumanne jioni baada ya kupatikana katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi ya Shauri Yako akiwa amejihami kwa panga na kisu.

•Maafisa wa polisi walimpata mshukiwa walipokuwa wanakagua kituo hicho baada ya shughuli za upigaji kura kukamilika.

Image: SCREENGRAB// CITIZEN DIGITAL

Polisi katika kaunti ya Homa Bay wanamzuilia mwanaume mmoja aliyepatikana na silaha katika kituo cha kupiga kura.

Mshukiwa alikamatwa Jumanne jioni baada ya kupatikana katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi ya Shauri Yako akiwa amejihami kwa panga na kisu.

Maafisa wa polisi walimpata mshukiwa walipokuwa wanakagua kituo hicho baada ya shughuli za upigaji kura kukamilika.

Baada ya kutiwa pingu mwanaume huyo alizidikishwa hadi kituo cha polisi kwa hatua zaidi kuchukuliwa.