Karua apiga kura, ahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi

Alitaja uchaguzi wa mwaka huu kuwa tofauti na ambao sauti za Wakenya zitasikika

Muhtasari

• Baada ya kupiga kura Kkarua alitoa wito kwa  Wakenya kujitokeza kwa wingi na kutekeleza haki yao ya kidemokrasia.

Mgombea mwenza wa urais wa Azimio la Umoja Martha Karua alipiga kura katika shule ya msingi ya Kimunye huko Gichugu, kaunti ya Kirinyaga mapema Jumanne. PICHA WANGECHI WANG'ONDU
Mgombea mwenza wa urais wa Azimio la Umoja Martha Karua alipiga kura katika shule ya msingi ya Kimunye huko Gichugu, kaunti ya Kirinyaga mapema Jumanne. PICHA WANGECHI WANG'ONDU

Mgombea mwenza wa urais wa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya Martha Karua amepiga kura katika eneo bunge la Gichugu, Kaunti ya Kirinyaga.

Bi Karua alipiga kura yake mapema sana wakati kituo cha kupigia kura kilipofunguliwa katika Shule ya Msingi ya Mugumoini eneo la Kimunye.

Baada ya kupiga kura Kkarua alitoa wito kwa  Wakenya kujitokeza kwa wingi na kutekeleza haki yao ya kidemokrasia.

"Nimepiga kura, kama unavyoona kutoka kwa wino kwenye kidole changu. Tafadhali, toka na upige kura. Leo ni siku yetu ya kuamua mwelekeo wa nchi hii, "alisema.

Alitaja uchaguzi wa mwaka huu kuwa tofauti na ambao sauti za Wakenya zitasikika. 

"Kuna uwezekano mkubwa kwamba kufikia jioni hii Wakenya watakuwa wameamua ni njia gani na nina hisia nzuri kuhusu leo." 

Karua ambaye alistahimili hali mbaya ya hewa ya baridi na manyunyu Kirinyaga hata hivyo alilazimika kuondoka kituo alichokuwa ameenda mapema baada ya kuelekezwa kwa kituo kingine cha kupigia kura kwa vile jina lake lilikosekana katika kituo cha kwanza.