Mgombea Ubunge Ikolomani Akamatwa na Maafisa wa GSU Akifanya Kampeni

Kukamatwa kuhusishwa na shambulio la usiku dhidi ya mpinzani wake wa ODM Bernard Shinali na kampeni haramu.

Muhtasari

• Ingawa polisi hawakutoa maelezo zaidi kuhusu kukamatwa, ripoti nyingine zilionyesha kuwa Butichi alikamatwa wakati akifanya kampeni usiku.
• Pia kulikuwa na ripoti kwamba angeweza kukamatwa wakati akiwahonga makarani wa kura.

Pingu
Image: Radio Jambo

Sheria za uchaguzi zipo wazi kwamba hakuna kupiga kampeni saa 48 kuelekea siku rasmi ya uchaguzi mkuu, na makataa hayo yalikamilika Jumamosi wikendi iliyopita ambapo wanasiasa walijikusanya maenneo mbali mbali kujinadi kwa mara ya mwisho.

Sasa imebainika kwamba mgombea ubunge eneo la Ikolomani, Khamisi Butichi anayegombea kwa tikiti ya ANC alikuwa anaendeleza kampeni chini kwa chini na kutiwa nguvuni na maafisa washika doria kutoka kitengo cha GSU nyumbani kwake.

Kukamatwa huko kulihusishwa na shambulio la usiku dhidi ya mpinzani wake wa ODM Bernard Shinali na kampeni haramu.

Msafara wa Shinali ulishambuliwa wakati ulikuwa ukizunguka eneo la Mukoyani alipokuwa akielekea nyumbani saa saba asubuhi.

"Alikamatwa na kuzuiliwa katika seli za Kakamega lakini anashughulikiwa na DCIO Kakamega Kusini," Daniel Ng'etich, CCIO Wa kaunti ndogo ya Kakamega ya kati alisema.

Ingawa polisi hawakutoa maelezo zaidi kuhusu kukamatwa, ripoti nyingine zilionyesha kuwa Butichi alikamatwa wakati alipokuwa katika muendelezo wa kufanya kampeni usiku.

Kuliripotiwa kwa shambulio kwa mshindani wake kuliripotiwa awali na baadae katika eneo bunge la Bumula, wagombeaji kutoka vyama vya UDA na DAP-K walishambuliana kwa risasi usiku wa kuamkia siku ya kura Agosti 9, machafuko ambayo yaliripotiwa kujeruhiwa kwa watu wanne huku wengine wkitoweka.

Katika mkasa huo uliotokea usiku, mwalimu mkuu aliyetambuliwa kama Walter Wanjala alikuwa miongoni mwa wanne waliojeruhiwa wakiwemo jamaa wengine waliotambuliwa kwa majina Joseph Wanyonyi, Simon Mayende, Munishi na Hesbon walijeruhiwa.