Twitter Yafungia Ujumbe wa Sifuna Ulioonesha Takwimu za Uongo za kura

Jedwali hilo lilionyesha kuwa Naibu Rais William Ruto alikuwa akifuata kwa takriban kura milioni 6.

Muhtasari

• Sifuna kwenye tweet hiyo, alikuwa ametuma jedwali lenye takwimu zinazoonyesha kuwa mgombea urais wa Azimio la Umoja alikuwa mbele kwa zaidi ya kura milioni 6.7.

Mgombea wa useneta wa Nairobi Edwin Sifuna wakati wa kibali Kasarani.
Mgombea wa useneta wa Nairobi Edwin Sifuna wakati wa kibali Kasarani.

Mtandao wa kijamii wa Twitter umeripoti na kuzuia ujumbe wa katibu mkuu wa ODM Edwin Sifuna.

Sifuna katika tweet hiyo alikuwa ametuma jedwali lenye takwimu zinazoonyesha kuwa mgombea urais wa Azimio la Umoja alikuwa mbele kwa asilimia 51.96.

Jedwali hilo lilionyesha kuwa Naibu Rais William Ruto alikuwa akishika mkia kwa 47.28%.

Baada ya kuona maelezo ya tweet, mtandao wa kijamii uliashiria kanusho, ikisema kuwa matokeo rasmi hayajatangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka.

Katika uchaguzi wa Kenya, vyombo vya habari na wagombea wanaruhusiwa kufanya hesabu zao.

Hata hivyo, kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais kumetengwa kwa mwenyekiti wa IEBC, na katika kesi hii ni Wafula Chebukati.