Otiende Amollo achaguliwa tena kuwa mbunge wa Rarieda

Ushindi wa Amollo unaashiria mwanzo wa muhula wake wa pili kama mbunge wa Rarieda.

Muhtasari

•Mbunge huyo alihifadhi kiti chake baada ya kupata kura 37,676 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Agustin Adhola aliyepata 23,266 chini ya chama cha United Democratic Movement (UDM).

Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo
Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo
Image: MAKTABA

Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo amehifadhi kiti chake.

Ushindi wa Amollo unaashiria mwanzo wa muhula wake wa pili kama mbunge wa Rarieda.

Mbunge huyo alihifadhi kiti chake baada ya kupata kura 37,676 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Agustin Adhola aliyepata 23,266 chini ya chama cha United Democratic Movement (UDM).

Amollo alikuwa akigombea kutumia tikiti ya Orange Democratic Party (ODM).

Wakili huyo wa mahakama kuu alikabidhiwa uteuzi wa moja kwa moja na chama cha ODM kwa sababu hakuwa na mshindani.

Alichaguliwa kwa mara ya kwanza kama mbunge wa eneo bunge la Rarieda katika uchaguzi mkuu wa 2017.Amollo alihudumu kama Ombudsman katika Tume ya haki ya utawala kwa miaka miwili kuanzia 2014 hadi 2016.