Azimio kufanya mkutano wa uzinduzi leo

Onsarigo alisema mkutano huo utafanyika KICC kuanzia saa nne alfajiri.

Muhtasari

•Muungano wa Azimio la Umoja utafanya kongamano la uzinduzi wa wanachama wake waliochaguliwa Jumamosi.

Image: Martha Karua/TWITTER

Muungano wa Azimio la Umoja utafanya kongamano la uzinduzi wa wanachama wake waliochaguliwa Jumamosi, katibu wa wanahabari wa Raila Odinga Dennis Onsarigo amesema. 

Onsarigo alisema mkutano huo utafanyika KICC kuanzia saa nne alfajiri.

Wahudhuriaji wameombwa kuvalia rangi za buluu za Azimio.

Azimio ameshinda viti 147 vya wabunge, viti saba vya Seneti na viti 10 vya ugavana kulingana na fomu zilizothibitishwa kufikia sasa.