Rais Uhuru Kenyatta asalia kimya baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu

Ni wiki moja sasa tangu Wakenya walipomuona ama kumsikia Rais Uhuru Kenyatta.

Muhtasari

• Alizungumza kwa ufupi na wanahabari Jumanne iliyopita baada ya kupiga kura.

Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta Rais Uhuru Kenyatta
Image: PSCU

Ni wiki moja sasa tangu Wakenya walipomuona ama kumsikia Rais Uhuru Kenyatta.

Alizungumza kwa ufupi na wanahabari Jumanne iliyopita baada ya kupiga kura katika mji aliozaliwa nje kidogo ya mji mkuu, Nairobi.

Alikuwa anamuunga mkono aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga kuchukua nafasi yake badala ya naibu wake, William Ruto, ambaye alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa Agosti 9.

Wawili hao walipochukua madaraka mwaka wa 2013 walikuwa na uhusiano wa karibu, kila mara wakiitana “kaka”, wakipiga makofi hadharani baada ya kutaniana na wakati mwingine kuwa na mahusiano ya karibu sana.

Haijulikani kwanini walikosana, lakini uhusiano wao ulizidi kuwa mbaya na kuzorota kuelekea siku za kuelekea uchaguzi wa mwaka huu ambapo walirushiana maneno makali.

Licha ya Bw Kenyatta kutokuonekana hadharani, serikali yake ilitangaza siku ya Jumanne  kwamba mchakato wa kumpata Rais mpya bado unaendelea.